Advertisements

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Fransic amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi uliochukuliwa na Uturuku kugeuza hekalu la Hagia Sophia lililopo mjini Instabul kuwa msikiti.

Akizungumza katika ibada moja makao makuu Vatcan kiongozi huyo aliongeza kuwa “mawazo yake yapo kwa watu wa Instabul”.

Hekalu la Hagia lilijengwa miaka 1500 iliyopita kwa ajili ya kutumiwa katika ibada za kikristo lakini baadae kugeuzwa kuwa msikiti baada ya mapinduzi ya Ottoman 1453.

Pia hekalu hilo lilitambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO kama sehemu ya kihistoria duniani na liligeuzwa kuwa makavazi ya kitaifa mwaka 1934 chini ya mwanzilishi wa Uturuki Padre Ataturk.

Mapema wiki hii mahakama ya Uturukui iliondoa hadhi hiyo ya kuwa makavazi ya kitaifa na kusema kuidhinisha matumizi mengine ya kuwa msikiti.

Advertisements

Papa Fransic amesema maneno machache kuhusu suala hilo “Mawazo yangu yawafikie wakazi wa Instabul, nikifikiria kuhusu Santa Sophia nasikia uchungu sana”

Aidha Rais Recep Tayyip Erdogan amesema ibada ya kwanza ya kiislam itafanyika Hagai Sophia Julai 24. huku muda mfupi baada ya tangazo hilo muito wa adhana ulisikika kwa mara ya kwanza kutoka katika hekalu hilo.

Pia vituo vya mtandao vya Hagai vimeondolewa mtandaoni.

Papa ni mmoja kati ya viongozi wakubwa duniani ambao wamekosoa vikali hatua hiyo, pia Baraza la Makanisa Duniani limetoa wito kwa rais Erdogan kubatilisha uamuzi huo.

Kanisa kubwa la kikiristo nchini Urusi ambalo lina idadi kubwa ya waumini wa dhehebu la Orthodox duniani, nalo limeeleza jinsi lilivyosikitishwa na uamuzi wa mahakama ya Uturuki likisema kuwa mahakama ya Uturuki haikutilia maanani maoni yake kabla ya kufanya maamuzi ya kuhusu keshi ya Hagai Sophia.

Advertisements

Pia Ugiriki nayo imekosoa vikali hatua hiyo, UNESCO imesema kuwa kamati ya kimataifa kuhusu maneneo ya kihistoria Duniani huenda ikatathmini upya thamani ya eneo hilo.

Mmoja wa waandishi maarufu wa Uturuki Orhan Pamuk ameiambia BBC kuwa hatua hiyo huenda ikaondoafahari waliyokuwa nayo Waturuki dhidi ya hiyo ya Kiislamu.

“Kuna mamilioni ya Waturuki ambao walipinga hatua hii kama mimi lakini sauti zao hazikusikika ” aliongeza Bwan Pamuk