Advertisements

Kocha Mkuu wa Manchester United amekiri kuwa klabu hiyo inastahili kile walichokipata baada ya kushindwa kuzipata pointi tatu katika mchezo uliopigwa dhidi ya Southampton.

Bao la Southampton la kusawazisha lililofungwa na Michael Obafemi katika dakika za lala salama limewafanya United kuikosa nafasi ya tatu na hatimaye kusalia katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi kuu Uingreza.

“Ni lazima ukubaliane na hilo kwani hata sisi tumewahi kushinda mechi nyingi kwa namna ile, ni sehemu ya mafunzo tu japo inaumiza kwani tayari ulishaamini kuwa pointi tatu ni zote zako” alisema Ole Gunnar.

Martial baada ya Mchezo kumalizika photo na Skysport

“Labda hatukustahili pointi tatu zote leo, wamecheza vizuri hila hatukua vizuri katika pasi tulizopiga baada ya kuongoza 2-1, japo tulijaribu kutengeneza nafasi na kucheza mchezo mzuri’ aliongeza Ole Gunnar

Advertisements

Magoli ya United yalifungwa na Marcus Rashford 23 pamoja na Anthony Martial katika dakika ya 23 huku mabao ya Southampton yakiwekwa wavuni na Armstrong 12 na Obafemi 90+6

Aidha Ole amemwagia sifa kipa wa klabu hiyo David De Gea akisema kuwa amejitahidi sana kulinda lango la United ila Southampton waliamkia upande mzuri kwa siku ya jana.

Southampton waliwatua Old Trafford wakiwa wakiwa na ushindi mkononi kutoka kwa Watford hali ambayo imewaweka pazuri kabla ya kuwavaa Mn U.

Advertisements
Advertisements