Frog AsdaHABARI

Maajabu, Chura alivyosafiri kisiri kwa ndege mpaka Uingereza

Advertisements

Chura wa kipekee aliyepewa jina la Asda amekutwa kwenye duka kubwa la kufanya manunuzi huko nchini Uingereza huku akiwa amesafiri umbali wa maili 5,000 kutoka Amerika ya kusini.

Dunia ina maajabu mengi sana katu huwezi kuyamaliza yote, utasikia hili na kusikia lile huku yote yakikuacha mdomo wazi. Mfanyakazi mmoja wa duka la Llanelli amembaini chura katikati ya ndizi ambazo zilikuwa zimewasilishwa ili kuuzwa kwa wateja.

Inasemekana kuwa chura huyo wa ajabu kutokana na uwezo wake ametokea nchni Colombia ambako mamia na maelfu ya tani za ndizi huzalishwa na kupelekwa Uingereza kila mwaka.

Kwa sasa timu ya uokozi ambayo ilifahamishwa uwepo wa chura huyo imearifu kuwa chura huyo ametunzwa katika eneo linaloitwa Pembrokeshire na anakula nyenji pamoja na nzi.

Aidha inasemekana kuwa wanyama aina ya amfibia wana uwezo wa kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula kutokana na hali ya hewa ya maeneo, na hiyo ndiyo inasemekana kuwa ni njia mojawapo iliyotumiwa na chura huy licha ya kusafiri umbali mrefu bila chakula wala maji katika halia ya hewa ya baraidi.

Hifadhi ya wanyama wa baharini yashukuru Asda kwa kumbaini na kumtunza chura huyo mpaka alipookolewa na kituo hiko picha BBC
Advertisements

Chura Asda wa sasa amehamishiwa katika kituo cha wanyama wa baharini kinachofahamika kama “Silent World Zoo To You” kituo muhimu cha wanyama wa baharini kilichopo huko Haverfordwest ambako kwa sasa atakuwa akiishi katika eneo la unyevu na mimea.

“Chura huyu wa pekee amesafiri maili 5,000 kwenye mikungu ya ndizi kutoka eneo lake la asili hadi duka la manunuzi la Llanellli bila shaka ni safair ndefu” amesema mkaguzi wa duka hilo Gemma Cooper.

Aidha Bi Coper ametoa shukrani zake kwa wafanyakazi wake kwa kumbaini Chura huyo na kumtunza hadi alipopokelewa

Advertisements

“kwa matunda yanayosafirishwa nje ya nchi jinsi yanavyopulizwa dawa na kutunzwa sio rahisi sio kawaida kuona chura au buibui akisafiri kwa kujibanza hadi sehemu iliyokusudiwa” amesema.

JE ZIPI NI SIFA ZA CHURA WA AINA HII?

  • Kwanza kabisa imebainika kuwepo kwa chura 800 wa aina hii huku zaidi ya 600 wakipatikana katika Amerika ya kati na kusini.
  • Vyura hawa hupatikana kwa rangi tofauti tofauti na baadhi yao huweza kubadilika rangi ili kuendana na mazingira.
Advertisements
  • Wengi wao huwa wadogo kiasi cha kuweka kuketi vizuri kwenye kidole kimoja cha mwanadamu.
  • Pia chura hawa hutumia macho yao ili kuweza kuwasaidia kula chakula, hufunga macho yao kabisa ili kusukuma chakula kipite kooni.
  • Baadhi, ngozi yao hutumika na watu ili kutengeneza dawa za kulevya.

SOMA PIA;

Categories: HABARI

Tagged as: , ,

1 reply »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.