Advertisements

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Q-chief ameweka wazi juu ya kizungumkuti kinachoendelea kuhusu kusaidiwa kwake na Harmonize ambaye ni CEO wa lebo ya Konde Music Worldwide.

Q-Chief amesema kuwa aliamua kujikataa kwa msanii huyo kufuatiwa na maneno maneno ambayo yalikuwa yakiongelewa kutokana na msaada aliopewa na Harmonize

Harmonize na Q-Chief wakati wanashoot video picha Eatv.tv

Q-Chief anasema kuwa Hamronize aliukuwa na nia njema ya kumsaidia pia alipenda harakati ila kama mtu mzima alielewa kuna vitu vinaendelea hivyo aliamua kujikataa ili kutovuja heshima na thamani ya kwa kuamua kukaa kimya

“Mdogo wangu alikuwa na dhamira nzuri na maamuzi, alitaka kufanya kitu kwa ajili ya kaka yake na nilipenda harakati zake, ila kumbuka nyuma yake kuna taasisi na watu ambao vimemzunguka, kwahiyo kuna muda kukwa na vitu vinaendelea au kuongeleka nyuma yangu ambavyo sivielewi au sivijui nikasema kutovunja heshima ya mtu aliyekupa thamani ni bora ukawa kimya nikajikataa”

Q-Chieft source eatv