HABARI

Dkt John Magufuli amteua Mama Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza

Advertisements

Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli amemchagua mama Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania kwa tiketi ya CCM,

Magufuli amemwagia sifa Mama Samia akisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano alichofanya nae kazi akiwa kama Makamu wa Rais, Mama Samia amejifunza mengi na angependa aendelee kuwa naye katika awamu ya pili.

“Katika kipindi nilichofanya kazi na mama Samia nimejifunza mambo mengi sana na kupitia yeye nawahakikishia nitakuwa mtetezi mzuri sana wa wanawake, nimekuwa nikimtuma popote hakatai kama nyie wanawake mkitumwa hamkatai” Amesema Magufuli.

Advertisements

Awali Magufuli aliwashukuru wajumbe wa mkutano Mkuu kwa kumchagua kwa asilimia 100 ambapo wajumbe wote 1822 walipiga kura za NDIYO.

“Wajumbe wamenipa heshima kubwa na nimebaki na deni kubwa, ninamuomba Mungu kura nilizopata leo zisinipe kiburi zisinifanye nijione wa muhimu sana bali zinipe nguvu nitumikie Watanzania wote” amesema Magufuli

“tupo kwenye nchi tajiri namimi ninataka kuhakikishia kama tukisimama kwa pamoja nchi yetu inaweza kuto machangio mkubwa sana duniani” aliongeza.

Chanzo: eatv

Categories: HABARI

Tagged as: , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.