Advertisements

Watu wengi wametoa maoni na masikitiko yao kufuatiwa na picha zinazosambaa mtandaoni zinazomuonesha official Shilole akiwa ameumia uso kutokana na kipigo ambacho ameeleza kuwa amekipata kutoka kwa mume wake, Uchebe

Moja kati ya watu ambao hawajakaa kimya na wameeamua kuweka wazi hisia zao juu ya kile wanachojisikia baada ya kuona picha hizo ni Waziri wenye dhamana ya Maliasili na Utalii nchini Mh Hamis Kigwangalla.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh Kigwangalla ameandika kuwa

“officialShilole amefanya nini kinachostahili kipigo chote hiki? hivi mwanaume ukishampiga hivi mkeo unaweza kumuambia tena ‘Nakupenda’? na kumuita tena honey, love, lawalawa, mk unavyompiga hivi unakuwa umepeleka wapi upendo, huruma ubinadamu na uanaume wako? hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo cha namna hii kwa mkeo Hakuna, Labda utuambie aliyetoa kipigo hiki hana aina mojawapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake kwa siku hiyo si vingine wanaume tuna wajibu wa kuwapenda kuwahurumia na kuwahudumia wake zetu tutimize wajibu wetu huu siyo vinginevyo kama unaona mwanamke amekushinda zungumza kumuacha au kumrudisha kwao ama kumruhusu aondoke lakini siyo kumpiga #Balozi wa wanawake #HK

Advertisements