Advertisements

Filamu nzuri ni ile ambayo imebeba mambo mengi ya kuvutia mfano waigizaji ambao wana uelewa mzuri na kile wanachokifanya, Naweza kusema kuwa filamu ya Kissing Booth ni moja kati ya filamu ambazo zimefanya vizuri sana kati ya filamu zinazohusisha maisha ya ujana.

Bila shaka watu wengi wametamani kuona tena waigizaji wao waliowapenda wakirudi tena katika Kissing Booth 2 ili kuamsha hisia kwa mara nyingine tena.

Netflix imeweka wazi kuwepo kwa Kissing Booth 2 ambayo itakuja kama muendelezo wa hadithi ya Elle, Noah na Lee, Tangazo ilo limetolewa kupitia katia ukurasa wa Twitter wa Netflix pamoja na ukuarasa wa twitter wa Joey King ambaye ameandika “Nina furaha, The Kissing Booth 2 inakuja Netflix Julai 24”.

Filamu ya Kissing Booth 2 itaongozwa na Vince Marcello na Jay S Anorld akiwa kama mwandishi wa mchezo, watu mahiri ambao waliiongoza Kissing Booth ya kwanza na kuifanya iwe filamu pendwa zaidi.

Advertisements

Licha ya kutolewa kwa tangazo hilo bado muongozo wa jinsi filamu hiyo itakavyokuwa haujawekwa wazi, aidha filamu ilimalizika kurekodiwa Agost 2019 na toka hapo imekuwa katika hatua za mwisho.

Los Angeles, California, na Cape town, South Africa ndizo sehemu ambazo filamu hii imerekodiwa.

Advertisements

#Sign Up ili kupata updates za movie