Advertisements

Binadamu tumeumbiwa uwezo wa kupenda vitu vingi tofauti tofauti kwa wakati mmoja, Mshambuliaji mahiri wa klabu ya Simba SC Meddie Kagere ameeleza mambo muhimu anayopenda kuyafanya akiwa nje ya uwanja.

Mnyarwanda huyo anasema kuwa kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi ni moja ya mambo muhimu anayopenda kuyafanya akiwa nje ya uwanja hasa vitabu vinavyohusu mafanikio ya kimaisha.

Pengine tunaweza sema tabia yake ya kusoma vitabu vya mafanikio inamjenga kufanya vizuri sana awapo uwanjani, na hata kupata mafanikio makubwa katika kucheza na nyavu kwani mpaka sasa Kagere ana jumla ya magoli 69.

Mbali na hapo ameisaidia Simba kufikia pointi 80 ikiwa imebakiza mechi tano kumaliza mzunguko wa pili katika msimu wa 2019/2020 Ligi Kuu Bara huku Meddi mwenyewe akiwa ametupia magoli 19 na pasi tano zilizozaa magoli.

Mpaka hivi sasa tayari timu ya Simba imeshakamilisha taratibu za kupata ubingwa baada ya kulazimisha sare na Tanzania Prisons na kufikisha pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote.

Advertisements

Julai 8 watakabidhiwa Kombe lao baada ya kumalizana na Namungo FC Mechi itakayopigwa katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa, Lindi.