Advertisements

Ukitoa orodha ya waandishi na waongozaji wa filamu zilizofanya vizuri sana sokoni Hollywood na duniani kote huwezi kumsahau James Cameroon, mmoja kati ya waongozaji na waandishi mahiri wa filamu zinazotumia teknolojia ya hali ya juu sana.

Titanic na Avatar ni miongoni kwa kazi zake ambazo zimechangia kumfanya awe na jina kubwa sana katika ulimwengu wa filamu duniani leo ebu tuangazie ukweli uliojificha katika Avatar 2009.

James Cameroon alianza kuandika filamu ya Avatar tangu 1994

Advertisements

Ilimchukua muda mrefu sana mpaka kufanikisha jukumu la kuileta Avatar kutoka katika mawazo yake Kituo cha Television cha ABC news kinaripoti kuwa baadhi ya picha ambazo zimetumika katika filamu ya Avatar zilianza kuonekana tangu miaka ya 1970, lakini ilitangazwa kuwa Cameroon alianza kutengeneza filamu hiyo kuanzia 1994.

Uduni wa teknolojia ndio uliomfanya Cameroon aendelee kusubiri huku akiziidi kuipa maboresho mbalimbali movie hiyo, alichokuwa anakitaka ni kusubiri mpaka teknolojia ya kutengeneza filamu zinazohusisha sayansi na mapambono (action) zitakapokuwa zaidi ndipo aachie filamu yake.

Muonekano wa Na’Vi umetokana na ndoto ya mama yake James Cameroon

Advertisements

Yapo mengi yaliyoandikwa na kusemwa kuhusu ugunduzi unaofanyika kila kukicha katika viwanda vya kutengeneza filamu, kuanzia katika kuumbwa kwa wahusika muonekano wao mpaka ushiriki wao inasemekena kuwa ni wa kubuniwa tu.

James Cameroon amewahi kueleza kuwa muonekano wa watu wa Na’vi waliokuwa wakiishi katika mwezi wa kughushi (Pandora) ulitokana na ndoto aliyoota mama yake ambayo alioneshwa mwanamke mrefu mwenye miguu kumi na mbili na mwili wake ukiwa na rangi ya buluu.

Pia Cameroon aliongeza kuwa hata muonekano wa The Terminator ya kwanza kabisa 1984 ilikuja kama ndoto alipokuwa akiiumwa huko Rome.

Mwanasayansi wa lugha, Paul Frommer ndiye aliyehusika kutengeza lugha iliyotumiwa na Na’Vi

Advertisements

Lugha nzuri inayoshangaza na kuvutia ni moja kati ya mambo ambayo huweza kufanya filamu ifanye vizuri sana katika mauzo, Huweza kuchukua hata karne moja ili kutengeneza lugha na kuanza kutumika miongoni mwa wanajamii. Mwanasayansi wa lugha kutoka chuo kikuu cha California Paul Frommer ndiye mhusika mkuu katika kutengeneza lugha iliyotumiwa na watu wa Pandora.

Baada ya Avatar kupata watuamiaji zaidi ilipofika 2005 Frommer aliamua kuongeza maneno 1000 zaidi ambayo yaliweza kutumia kama sehemu ya lugha hiyo,

Milio na Sauti za wanyama walioishi Pandora zimetokana na wanyama wasio wa kufikirika

Advertisements

Tukiwa tunaangalia filamu ya Avatar tunaweza kusikia sauti tofauti tofauti ambazo ukizitilia maanani unaweza kugundua kuwa ni wanyama, wadudu pamoja na ndege, Kampuni ya SkyWalker Sound ndiyo kampuni iliyohusika katika kutengeneza milio ya wanyama inayopataikana ndani ya movie ya Avatar.

Juan Peralta designer aliyehusika na masuala ya sauti anaeleza kuwa sauti za Mbwa mwitu, Mbwa, nyoka zilitumika pia sauti za Fisi zilizorekodiwa kutoka Costa Rica na Afrika zimetumika katika kutengeza filamu hiyo.

Lugha ya Na’Vi imetokana na lugha ya Kipersia Kichina na Kimhariki.

Paul Frommer ambaye ndiye mwanasayansi aliyehusika katika kutengeneza lugha iliyotumika na Na’Vi alitumia lugha tatu kuziunganisha na kupata lugha moja.

Kimhariki ambayo ni lugha ya Taifa ya nchi ya Ethiopia, pia lugha kutoka Amerika na aAsia ya kati “baadhi ya lugha zingine ambazo nilikumbana nazo ni lugha ya Kipersia ambayo inafanana na Kichina au Kiindoneshia au Kiebrania l;akini muunganiko wake ni wa ajabu na kipekee mno” alisema Paul Frommer.

“Mpaka sasa kuna zaidi ya maneno 40,000” aliongeza Frommer, mashabiki pia bado wanaendelea kujifunza kuandika na kuongea lugha hiyo.

Frommer anasema kuwa hakutaka kuiweka lugha hiyo rahisi kujiunza bali alitaka iwe kama shindano kwa mashabiki ambalo linawezekana kufaulu

SHARE