Advertisements

Benki ya Dunia imeiorodhesha Tanzania kama nchi yenye uchumi wa kati siku ya Tarehe 1 Julai 2020, hatua inayojiri mapema zaidi ya muda ambao ulipangwa na Rais John Magufuli.

Akiwa anaingia madarakani aliweka ahadi kuwa mpaka kufikia 2025 atakuwa ameweza kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye uchumi wa kati, lakini uwezo wake wa kufanya kazi umeliwezesha Taifa hilo kufikia vigezo vya uchumi wa kati kabla ya kufikia 2025.

Rais Magufuli amewapongeza Watanzania kwa juhudi walizozifanya hadi kufikia hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika kuwa ” Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai 2020 imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI. Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio hata. Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020 MUNGU IBARIKI TANZANIA”

Advertisements

VIGEZO VILIVYOANGALIWA

Deus Kibamba ni mchanganuzi wa masuala ya Uchumi kutoka Tanzania naye anasema kuwa, Benki ya Dunia huangalia pato la Taifa kwa mfano kupitia jumla ya utajiri ule wa rasilimali na ule wa kifedha na kugawanya na watu wa Tanzania.

Pia anasema kuwa “Mataifa yenye kipato cha dola kati ya 1,006 hadi 3,955 kwa mtu mmoja hutajwa kuwa mataifa ya kipato cha kati, lakini yaliyo na uchumi mdogo. Yale yaliyo na dola kati ya 3,958 hadi 12,235 yanadaiwa kama mataifa yenye kipato cha kati yaliyoimarika.”

Advertisements

“Taifa la Tanzania hivi sasa linaelekea kukua kiuchumi kwani ishara za siasa ya taifa hilo zinaenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa taifa hilo na kwamba sifa hiyo italiongezea taifa hilo zaidi uwekezaji wa kigeni hatua ambayo italifanya kuimarika zaidi kiuchumi” aliongeza Kibamba.

Hata hivyo hatua hii haiwafanyi Watanzania waanze kufikiri kuwa mifuko yao itaanza kufaidika kutokana na hilo na badala yake wanatakiwa kufanya bidii zaidi hili kuimarisha uchumi.

Advertisements

Kulingana na Kibamba anasema kuwa hatua ya uongozi uliopo kudhibiti matumizi ya fedha mbali na kukabiliana na uvujaji wa fedha ni miongoni mwa hatua muhimu zilizochukuliwa na serikali hiyo kufikia malengo yaliyotarajiwa 2025