Advertisements

Timo Werner nyota anayechezea klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundersliga, amesema kuwa anaweza kusaini klabu yoyote ambayo inahitaji saini yake kwa sasa hila kwa vigezo maalum.

Manchester United, Inter Milan, Liverpool pamoja na Chelsea Zimetajwa kumpigia mahesabu nyota huyo mwenye miaka 24 huku Chelsea ikipewa nafasi kuwa katika kuwahi saini ya Werner.

Timo ameeleza kuwa fedha sio jambo la muhimu sana kwake ila anachotazama yeye ni malengo ya timu kufika mbali na kutwaa ubingwa.

“Fedha kwangu sio sababu ya mimi kwenda kucheza ama kusaini ingekuwa hivyo ningependa kucheza China, ila kwa kuwa Chelsea, Liverpool na United sawa ninaweza kusaini kwa timu ambayo itakuwa bora kwangu” alisema

Advertisements