Advertisements

Ligi kuu ya Uingereza (EPL) pamoja na kombe la Ligi nchini humo kwa kushirikiana na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) wameuweka wazi mpango wao mpya unaotoa nafasi za kufundisha kwa makocha weusi wanaotoka katika bara la Asia na na nchi zingine ambazo hazijapiga hatua kuwa katika soka.

Kocha wa Doncaster Rovers Dorren Moore ambaye ni mshauri maalum wa mipango ya watu weusi Ligi kuu Uingereza amesema kuwa utaratibu huo utaanza katika msimu huu wa 2020.

Mwanafunzi atatua fumbo la hisabati lililosumbua kwa miaka 50 ndani ya wiki moja

Utaratibu huo amabo utaanza msimu ujuao unawapa naasi makocha sita wanaotoka katika nchi za (BAME) kujumuika katika benchi la ufundi msimu mzima katika vilabu kadhaa vinavyoshiriki ligi kuu Uingereza.

Advertisements

Hadi kufikia hivi sasa ni makocha sita tu kutoka katika nchi za BAME ambao wanafundisha kama makocha wakuu katika vilabu 91 ya EPL na EFL Hivyo mpango huu unatarajia kuongeza idadi.

VIGEZO NA MASHARTI

Advertisements
  1. Mpango huo unafadhiliwa na chama cha soka Uingereza FA pamoja na PFA unamtaka kocha awe na leseni B ya ukocha inayotambulika na shirikisho la soka barani ulaya UEFA.
  2. Kocha anayeomba kuingia katika mafunzo haya anatakiwa awe tayari ameshaanza mafunzo ya kupata leseni A ya ukocha ya UEFA
  3. Awe ameshiriki FA Advanced Youth Awardna kupitia majaribio kadhaa katika vilabu tofauti tofauti