Advertisements

Meneja wa Liverpool FC Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool haiwezi kutumia mamilioni ya fedha ili kusajili viungo wapya kuchezea klabu hiyo kwani bado wao wenyewe wanajiweza vizuri.

Hivi karibuni Liverpool wametangazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu ya Uingereza jambo ambalo limempa hehima kubwa sana Klopp, mashabiki wengi walitegemea kuwa Klopp angafanya usajili wa kufa mtu ili kujipanga kuchukua ubingwa mara ya pili kwa msimu ujao hila imekuwa tofauti.

Werner akubali kutua Chelsea, Machester United na Liverpool kwa vigezo

Kwani mpaka sasa tayari Liverpool imeshajitenga mbali katika kuwania saini ya nyota kutoka RB Leipzig ya Ujerumani Timo Werner kwa Euro Milioni 50, jambo ambalo limewapa shibe wapinzani wao Chelsea na Man United katika kushinda saini ya nyota huyo.

“Sisi hatuna wachezaji 11 wanaoweza kuanza bali tuna wachezaji 16 au 17 wanaoweza kuanza, hatuwezi kutumia mamilioni na mamilion kusajili” Amesema Klopp

Wachezaji wa Liverpool

Ikumbukwe kuwa tangu Liverpool walipotumia kiasi cha Euro milioni 65 kumnasa golikipa Allison Becker 2018 hawakuhiatji tena kutumia fedha nyingi katika usajili.

Klopp amesema kuwa ataendelea kuwakuza nyota wadogo walioko katika klabu hiyo “Tunahitaji kukihimarisha kikosi, na hiki kikosi ni himara tayari, lakini tatizo la kikosi imara ni pale unapohitaji kukihimarisha zaidi kwa ajili ya mauzo sokoni” amesema Klopp

Advertisements

Untakiwa kutumia fedha ili kufanikisha hilo, lakini ukweli ni kwamba si pesa pekee unatakiwa kuwa mbunifu, nasi tunajaribu kuwa hivyo tunajaribu kutatua matatizo ya ndani mpaka tufikie huko, bila shaka tuna wachezaji watatu au wanne ambao wanaweza kufanya makubwa” aliongezea.

Gabo Zigamba aweka wazi sababu ya kufunga ndo kwa siri

Harvey Elliot mmoja kati ya nyota wadogo kutoka Liverpool, picha na Skysport
Advertisements