Advertisements

Msanii wa filamu nchini Tanzania Gabo Zigamba amefunguka sababu ya kufunga ndoa kwa siri na kusema kuwa mambo ya ndoa ni ya mtu binafsi na huwa hapendi kuweka wazi ama kuzungumzia jambo hilo.

Taarifa za msanii huyo kufunga ndoa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii April 21 akiwa amevalia mavazi na akiwa katika mazingira ambayo yaliashiria kuwa alikuwa anafunga ndoa

Akizungumzia suala hilo kupitia EATV& EA Radio Digital zigamba ameeleza kuwa “huwa sipendi kuzungumzia hivyo vitu kwasababu kuna vitu viwili, kwanza mtu anayeniona anatafuta uhamasishaji kutoka kwangu, sasa kuhusu ndoa siwezi kumhimiza mtu na haifanani kabisa sawa na duka la vipodozi kwenda kuulizia sigara”

Advertisements

“Pili suala la mimi kuoa au kutooa kwa mtu ambaye anamfuatilia Gabo Zigamba haimsaidii chochote, kuoa, kuolewa au kufanya maulid haina uzito wowote kwa jamii hayo ni mambo ya mtu binafasi japo ulaya wanafanya sana hizo style. Kwa sisi bado hasa ukiangalia soko letu halipo sana rasmi, kuna vitu vingi vya kupiga kelele ili tuweze kusogea”. Gabo aliongeza

Advertisements