Advertisements

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanatarajiwa kushusha majembe mapya ya kazi msimu ujao na hivyo hakuna nafasi ya kuendelea kulizungumzia suala lamchezaji wao Bernard Morrison.

Tangu awali kumekuwa na mvutano kati ya Morrison pamoja na klabu yake ya Yanga kuhusu mkataba uliowekwa huku Morrison akisema kuwa mkataba wake unaisha msimu huu, na Yanga wakisema kuwa hawatambui kauli yake wanachojua ni kwamba wana mkataba nae wa miaka miwili.

Aidha Mwakalebela ameweka wazi kuwa wanahitaji kufanya usajili ulio makini na wa kiwango cha juu msimu ujao ili kuepuka changamoto za hapa na pale kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo pamoja na timu kuwa kiwango cha chini.

Advertisements

“kwa sasa mtazamo wetu haupo kwa Morrison kuna mambo mengi ya kufanya na kuyazungumzia katika klabu yetu ya Yangna kuliko kumzungumzia yeye” alisema Mwakalebela.

“Tunajipanga kuhakikisha tunakuwa makini zaidi kufanya usajili msimu ujao wa ligi kuu, tuanhitaji kuwa na kikosi kipana na imara cha ubingwa kila mchezaji atakayepata nafasi ya kuchaguliwa ni lazima awe anapata nafasi katika timu aliyotokea” Aliongeza.

“Kwa sasa tunajipanga ili kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi zote zilizo mbele yetu na ule mchezo wa FA ili kupata nafasi ya kushiriki mechi za kimataifa mwakani”. alimalizia.