Traditional Medicine ChineseHABARI

China yageukia mitishamba ili kutibu Corona

Wakati dunia nzima ikiwa imesimama ili kukomboa mataifa yote kutoka katika janga la corona China, Taifa ambalo kwa muda mrefu limekuwa kinara kwa utengenezaji wa dawa za asili limeamua kugeukia dawa za asili ili kuweza kutibu ugonjwa wa corona.

China imetengeneza dawa inayoitwa “Tradional Chinese Medicine” ambayo mpaka sasa imetibu 92% ya wagonjwa wa corona nchini humo.

Gazeti moja lililozinduliwa na serikali ya China linathibitisha kuwa TCM ni dawa ya kale zaidi duniani ambayo imetengenezwa kwa mitishamba, pia licha ya kuzua mijadala mingi sana mitandaoni bado dawa hiyo imekuwa maarufu.

Rais XI anasemekana kuuunga mkono dawa za mitishamba

Serikali ya China imeweka kitengo maalum cha TCM kinachowezesha kukabiliana na ugonjwa wa corona huku ikidaiwa kuwa dawa hiyo imesaidia sana kutibu ugonjwa SARS miaka mingi iliyopita nchini humo.

Wanasayansi duniani bado wana mashaka kuunga mkono suala la China kuidhinisha matumizi ya TCM iili kutibu ugonjwa wa corona, licha ya watu kutoa ushuhuda kuwa hakuna madhara ukitumia dawa hiyo bado wanasayansi wanasisitiza uchunguzi wa kisayansi ufanyike.

Advertisements

Taasii ya Afya nchini Marekani ilisema kuwa dawa hiyo itasaidia kuondoa dalili za ugonjwa huo lakini sio kutibu moja kwa moja.

Mtafiti wa zamani wa Uingereza wa dawa ambazo zimeunganishwa Dk Edzard Ernst alinukuliwa akisema kuwa “hakuna ushahidi wowote mzuri ambao unaweza kuthibitisha matumizi yake hivyokuna hatari ambayo bado haijaweza kuelezewa.

Licha ya vipingamizi vyote bado TCM inaendelea kupata umaarufu nchini China huku kukionekana kuna uhitaji mkubwa kimataifa.

Advertisements

Baraza la Taifa la China mwaka jana lilikadiria kiwanda cha TCM kingegharimu kiasi cha dola bilioni 420 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.

Rais XI anasisitiza kuwa watu wake wa China wanaipenda dawa hiyo na kuiona kama hazina ya China iliyoachwa enzi za mababu kwa mababu.

1 reply »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.