Binti wa Beyonce na Jay Z anayejulikana kwa jina la Blue Ivy Carter ameshinda tuzo za BET 2020 zilizofanyika June 28 kwa mara ya kwanza kupitia wimbo wake wa ‘Brown skin girl’
Wimbo wa Brown Skin Girl uliwekwa katika kategoria moja na wimbo wa “Underdog wa Alicia Keys, Melanin wa Ciara, Luita Nyong’o, Ester Dean, City Girls and La La, I choose wa Layton Green pia Tempo wa Lizzo na Missy Eliot na Afeni ulioimbwa na Rhapsody na PJ Morgan.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza Blue Ivy kupewa nafasi kuwania tuzo mbalimbali kupitia wimbo huu ambao uliimbwa kwa ajii ya zawadi katika filamu ya The Lion King 2019.
Ukiachana na tuzo ya BET ambayo imejinyakulia June 28, nyimbo hii pia imeweza kukshinda tuzo za NAACP Image Award kama nyimbo bora ya kutumbuiza pia tuzo za uandishi bora za Ashford na Simpson.

Usiku wa Tuzo za BET umekuwa usiku mzuri sana kwa familia ya Carters kwani Beyonce naye aliweza kutunukiwa tuzo ya heshima ya Ubinadamu, pia albamu yake ya Homecoming the live Album kuingia katika kategoria ya kuwania albamu bora ya mwaka, Msanii bora wa R&B wa kike, na filamu bora ya mwaka ambapo Homecoming:Afilm by Beyonce ilishindanishwa.
Mashabiki wa Blue Ivy nao hawakuwa nyuma katika kufurahia ushindi alioupata msanii huyo ambaye kwa sasa tunawea kusema kuwa anafuata nyao za wazazi wake.
ONA PICHA





Categories: HABARI