Msanii na mwigizaji kutoka nchini Nigeria Peter Okoye maarufu kama Mr P amethibitisha kuwa yeye pamoja na familia yake wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Msanii huyo ameweka wazi kupitia video aliyoipakia katika ukurasa wake wa instagram akithibitisha kuwa yeye, mkewe Lola Omotayo pamoja na binti yake Aliona wamekutwa na maambukizi ya virusi hivyo

“Mkewangu, binti yangu na mimi mwenyewe tumekutwa na maambukizi ya virusi vya corona” Mr P ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram

Kupitia chapisho lake katika ukurasa wa twitter Mr P amewahusia mashabiki zake kutulia nyumbani pia kuwa salama.

Advertisements
chapisho la Mr P kutoka katika mtandao wa Instagram