Klabu ya Liverpool imelaani vikali baadhi ya tabia zilizooneshwa na mashabiki wao waliokusanyika mijini wakati wakisherehekea ubingwa uliotwaliwa na klabu hiyo.

Mashabiki wa Liverpool walikusanyika katika eneo la kihistoria la Liverpool linaloitwa Pier Head Waterfont huku wakichoma gesi pamoja na kulipua mafataki licha ya kuwepo kwa sheria inayokataza mikusanyiko ya watu katika jiji hilo.

Meya wa jiji hilo Joe Anderson amesema kuwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa klabu ya Liverpool kimeleta aibu kwa timu hiyo pamoja na jiji la Liverpool kwa ujumla”

Aidha maneno hayo yametiliwa mkazo na klabu ya Liverpool baada ya kusema kuwa “Jiji letu lipo katika janga la kiafya na tabia hizi hazikubaliki, Mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona umefikia kileleni, na sote tunahitajika kushirikiana ili kuhakikisha kuwa hatupotezi maana ya kuwa ‘lockdown’.

“Itakapokuwa salama kufanya hivyo basi tutakusanyika kwa pamoja kusherehekea ubingwa ambapo kila mmoja anaweza kuhudhuria: Liverpool FC iliongeza

Meya Anderson ameiambia BBC asilimia 95 ya mashabiki walikuwa wamesikiliza ombi la serikali yao kuwa hawatakiwi kukusanyika pamoja lakini wametokea wachache ambao wamelichafua jina la Liverpool

Advertisements
Eneo la tukio

Hali kama inavyoonekana kwenye picha hili ni baada ya kumalizika kwa sherehe na fujo zilizofanywa na mashabikiwa Liverpool.

Advertisements

Unaweza kuona takataka za vyupa vilivyokwishatumika, keni za kuhifadhia gas zilizotumika mifuko na karatasi zilizochakaa.