Mwanamume aliyejulikana kwa jina la Munala (42) kutoka nchini Kenya amefariki dunia kutokana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya Viagra.

Mwanamume huyo ni mkazi wa mjini Kakamega, naye aliaga dunia asubuhi ya Jumatano Juni 24 akidaiwa kutumia dawa za kuongeza ashiki za kimapenzi kupita kiasi.

Afisa Kiongozi wa Polisi wa Kakamega, David Kabena amesema kuwa mwathiriwa alikodisha chumba katika hoteli moja iliyofahamika kwa jina la Amazon akiwa na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Anyango (31) siku ya Juni 23 mchana.

Advertisements

“Wawili hao waliagiza chakula kutoka katika hoteli hiyo ila mwanamke huyo ndiye alikuwa amekula, asubuhi yake mwanamke alitoka na kumfuata meneja wa hoteli hiyo na kumwambia kuwa mpenzi wake amefariki dunia baada ya kutumia dawa za kupandisha ashiki za kimapezi aina ya viagra kupita kiasi”

Afisa huyo wa Polisi ameongeza kuwa, “Meneja aliwaita maafisa wa polisi kisha kuuupeleka mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa na mafunzo mjini Kakamega ambapo ulifanyiwa upasuaji, na matokeo ya upasuaji yalionesha kuwa marehemu alifariki kutokana na mshtuko wa moyo uliosababishwa na matumizi ya dawa hizo”

Chanzo TukoNews, Kenya