Mwanafunzi mmoja anayesoma chuo Kikuu cha Texas nchini Marekani amefanikiwa kutatua fumbo la hisabati lililopasua vichwa vya wanahisabati mashuhuri duniani kwa zaidi ya miaka 50.

Mwanafunzi huyo anayejulika na kwa jina la Lisa Piccirillo amekuwa akifanyia kazi shahada ya ya udaktari katika chuo hicho, wakati alipoweza kutatua fumbo la hisabati la Conway kwa muda wa wiki moja.

Tatizo hilo la hesabu la Conway lilipendekezwa na mwahisabati wa Uingereza John Horton Conway 1970, lakini Lisa Piccirillo alisikika kwa mara ya kwanza katika warsha moja 2018

Profesa Gordon anasema kuwa ” sidhani kama alikuwa amefahamu hesabu hiyo ilikuwa maarufu sana zamani”

Kazi ya Bi Piccirillo ilichapishwa mapema mwaka huu katika jarida la hisabati lililoitwa Annals Mathematics na tangu hapo akafanywa kuwa naibu profesa katika taasisi ya teknolojia ya Massachusetts

Fumbo la Conway lilikuwa halijatatuliwa kwa muda mrefu

Kulingana na Mtafiti Chuo Kikuu Cha Madrid na mwanachama wa taasisi ya hisabati ya Uhispania ICMAT Javiwe Aramayona anasema kuwa fumbo la Conway ni la muda mrefu mno na wanahisababti werevu wengi duniani wameshindwa kulitatuta.

Aidha anasema kuwa Topology (elimu ya utafiti kuhusu tabia ya vitu vikiundwa, kukunjwa na kuvutwa bila kuvunjika) ni muhimu katika sekta nyingi za sayansi na imetumika na wanasayansi kutafiti tabia za vitu katika masoko tofauti na maumbile za molekyuli za jeni.

#Get us on

JOHN HORTON CONWAY NI NANI?

John Horton Conway ni mtu aliyevumbua fumbo hilo la kamba, alifariki April akiwa na umri wa miaka 82.

Amezaliwa eneo la Liverpool na ni mtaalam wa masuala ya hisabati mwenye ushawishi mkubwa akiwa anafanya kazi katika vyuo vikuu vikubwa kama vile Cambridge na Princeton.

Mwandishi wa biografia Bwana Siobhan Roberts yake anasema kuwa Horton ni sawa na “Archimedes, Mick Jigger, Salvador Dali na Richard Feyman wakikusanywa pamoja na kuwa mtu mmoja, pia alikuwa ni mtu ambaye alipendwa zaidi na ulimwengu.

Mwanahisabati John Horton Conway

Bi Piccirillo aliweza kutatua fumbo la hesabu ya Conway ambalo lina misalaba au mikunjo 11 kwa kutengeneza toleo linalofanana na hilo ambalo linajulikana kama “fundo la ndugu” ambalo lilimrahisishia kidogo kujifunza.

Kwa kutengeneza fundo hilo na kulitatua aliweza kutumia matokeo yake na kulitatua fumbo la Conway

“Sikujiruhusu kulitatua fumbo hilo wakati wa mchana kwa sababu sikuona kama ni hesabu halisi, nilidhani ilikuwa ni kama kazi yangu ya nyumbani kwa hiyo nilienda nyumbani na kuifanya

Bi Piccirllo akiliambia gazeti la Quanta