Mwandishi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki Khaled Mohammed Khaled almaarufu kama DJ Khaled kutoka nchini Marekani ameshtua mioyo ya mashabiki wake duniani baada ya kutangaza nia yake ya kustaafu muziki na kuishi kama wakali wegine wa muziki nchini humo.
Mtayarishaji huyo ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kustaafu muziki na kuwa kama Jay Z au Michael Jordan kwa upande wa mchezo wa NBA.
“Ningeweza kustaafu kama walivyofanya Jay Z na Michael Jordan walivyofanya muda wowote ambao ningetaka, naweza kustaafu leo na kufurahia yale yote niliyoyatimiza na kuendelea kupokea baraka na upendo zaidi” ameandika DJ Khalid.
“Nina shauku ya kushea baraka nyingi, kuwashawishi na kuwahamasisha vijjana wengine kwenye ulimwengu kote, najihisi kama Jay Z au Michel Jordan” aliongeza DJ Khaled.
DJ Khaled alianza kazi yake ya muziki mwaka 2006 alipotoa albamu yake ya kwanza iliyoenda kwa jina la “Listenn” akiwashirikisha wasanii wakubwa Marekani na duniani kote kama vile Nicki Minaj, Birdman, Lily Wayne, Meek Mill, Chris Brown na wengineo wengi duniani kote.
- Babalevo atangaza vita kwa yeyote atakayemtukana Diamond
- Masaa 36 ya mfungwa namba 8612- Doug Korpi
- Samatta ajiunga na Fenerbahce, Aston Villa FC yashuka followers
- Tanzania: Panya anayeweza kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini, atuzwa
- Swizz Beatz afunguka sababu za Diamond kuimba Kiduchu kwenye Wasted Energy
Categories: HABARI