Timu ya Singida United bado imeendelea kuwa wenye hali tete baada ya kushindwa kuibuka kidedea katika mchezo uliopigwa dhidi ya JKT Tanzania hapo Juni 20.

JKT Tanzania iliwafunga mabao 2-0 Singida United, mabao ambayo yalifungwa na Musa Said dakika ya 11 na Hafidh Mussa dakika ya 61.

Ofisa Habari wa Singida united Calse Katemana amesema kuwa “mapumziko ya corona yaliwafanya washindwe kufanya vizuri ila wana imani ya kurejea kwenye ubora wao”

“Tulianza kwenye ubora kabla ya corona tuliwafunga Mbeya City hicho ndicho ambacho tunakitaka ila kwa sasa tunaanza kujipanga upya maana corona ilituvuruga aliongeza

Hivi sasa Singida United ipo katika hatari ya kushuka daraja huku ikiwa imeshika nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo 30.

Chanzo SaleheJembe