Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ameagiza vijana wa JWTZ kuhakikisha Lori lililozama Mto Wami linatolewa mara moja.

Jen. Mabeyo amesema hayo baada ya kuguswa na majanga yaliyomkuta Bi Mwajuma Selemani mmiliki wa Lori lililozama Mto Wami kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Kikosi cha uokoaji kutoka JWTZ kimefika Wami kikiwa na gari mbili za uokoaji na kimefanikiwa kulichomoa Lori hilo leo, jambo ambalo lilishindikana kwa waokoaji wa kwanza kutokana na madai kwamba kina ni kirefu, kasi ya maji maji machafu nk hadi kumfanya mwajuma akate tamaa na kurusi DSM.

Hata hivyo timu ya JWTZ iliyohusika na uokozi wa lori hilo inasema kuwa bado injini na kibini havijapatikana licha ya wazamiaji kuvitafuta kwa nguvu zote.

“Mzigo tumeshindwa kuupata umekwenda na maji injini na kibini vinaonekana baada ya gari kugeuzwa vilichomoka na havijaonekana, Mkuu wa Majeshi amefanya kwa nafasi yake lakini naamini wapo Watanzania watafanya msaada zaidi ya hapa” alisema Kapteni Obedy Mwakalobo akizungumza kupitia Ayotv

Chanzo Ayotv