Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Azam FC watapambana vikali kuhakikisha wanaibuka na ushindi wa pointi tatu zote.

Katika mchezo wa uliopita Azam FC waliondoka na pointi tatu dhidi ya Yanga baada ya kuwachapa 1-0

Eymael amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya

“Kila kitu kipo sawa na tutakamilisha ushindi kwa kucheza mpira wa pasi na kutulia, tunakumbuka kuwa mchezo wa kwanza walitufunga ila sasa hatutakubali kufungwa tena”

“Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti ili kuona namna gani timu itapata matokeo kwenye mchezo wetu mgumu alisema Eymael

Yanga itashuka katika dimba la Taifa kumenyana na Azam FC saa 10:00 jioni

Chanzo SaleheJembe