Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam Fc Bwana Thabit Zakaria maarufu kama ‘zakazakazi’ leo hii ameamua kuweka wazi udhaifu wa klabu ya Yanga.

Aidha msemaji huyo ameeleza jinsi Azam FC watakavyoibuka na ushindi katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa jioni ya leo katika dimba la Taifa

“Yanga imezifunga timu nyingine mara nyingi zaidi kuliko ilivyoifunga Azam FC tumeifunga mara 8 nao wametufunga mara 8 kati ya mara 23 tulizokutana katika ligi, hivyo leo tutawafunga mara ya tisa na kuwaacha na idadi yao” alisema Zakazakazi

“Yanga haina kikosi cha ushindani ndio maana inatoa sana morali ya fedha kwa wachezaji iliw apate ushindi, ninawaambia hizo pesa bora wakatoe hata misaada maana hawatapata ushindi. ameongeza

Azam FC kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 kati ya michezo 29 huku Yanga ikiwa na pointi 55 nafasi ya tatu kwa michezo hiyohiyo 29.