MICHEZO

Arteta: Kichapo dhidi ya Brighton ni kosa letu

Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amekiri kuwa kichapo walichokipata dhidi ya Brighton ni kosa lao wao wenyewe kwa kushindwa kucheza soka kama ilivyohitajika.

Kocha huyo ameeleza kuwa klabu yake inastahili kulaumiwa kwa kichapo walichokipata katika dakika za lala salama,

“Nafikiri tulifanya mambo mengi ili kupata ushindi, lakini hatukushindana kama unavyohitajika katika Ligi kuu ya Premier, tuliweza kupata goli la kwanza kama ilivyokuwa lakini mbeleni tukapoteza msimamo. yote ni makosa yetu” Arteta alisema baada ya mchezo kumalizika

Katika mchezo huo Arsenal walikuwa wa kwanza kujipatia bao katika dakika ya 68 lililofungwa na Nicolas Pepe, lakini hata hivyo bao hilo halikuweza kuwafanya waibuke washindi.

Dakika ya 75, Lewis Dunk aliweza kusawazisha kwa kuipatia Brighton bao la kwanza, huku Neal Maupay akitikisa tena wavu wa Arseanal katika dakika za nyongeza.

1 reply »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.