Wakati Wagombea mbalimbali wakiwa wanatangaza nia zao ili kuwania viti tofauti tofauti katika uchaguzi mkuu 2020, Msanii wa Hip Hop anayejulikana kwa jina la Wakazi ameamua kutupa karata yake kwenye siasa.

Msanii huyo ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Ukonga kupitia chama cha ACT Wazalendo kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakazi ameeleza nia yake ya kuliongoza jimbo hilo leo tarehe 20, 2020 katika mkutano wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es salaam.

Licha ya yote amesema kuwa, amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu hivyo sasa ni wakati wa kuwa kiongozi.

kwasababu nimepata heshima ya kuitwa hapa mbele ya mkutano naomba nitumie nafasi hii kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo langu la Ukonga”

Hivi karibuni mkali huyo wa Kanda maalum alikabidhiwa kadi ya chama cha ACT Wazalendo na kiongozi Mkuu wa chama hicho Zitto Zuberi Kabwe

Chanzo: Mwanahalisionline

#Show love with us