Ni ajabu kusikia kuwa Jogoo ameshtakiwa kwa kosa la kuwika kila asubuhi, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Jogoo ambaye anajulikana kwa jina la Maurice baada ya kushtakiwa mahakamani na wanadoa wastaafu waliokuwa wakiishi nchini Ufaransa katika kisiwa cha Oleron.

Ni ajabu kusikia kuwa Jogoo ameshtakiwa kwa kosa la kuwika kila asubuhi, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Jogoo ambaye anajulikana kwa jina la Maurice baada ya kushtakiwa mahakamani na wanadoa wastaafu waliokuwa wakiishi nchini Ufaransa katika kisiwa cha Oleron.

Mmiliki wa jogoo hilo Corinne Fesseau anakana mashtaka hayo kwa kusema kuwa alichokuwa anafanya jogoo wake ni kuwika kawaida tu kama jogoo wengine, jambo lingine la kushangaza ni kwamba Jogoo Maurice pamoja na waliomshtaki hakuna aliyekuwepo mahakamani ana kwa ana wakati kesi hiyo ikisikilizwa

Jogoo Maurice ameanza kupata umaarufu kimataifa na kuwa nembo ambayo inatumika kulinda sauti nchini Ufaransa baada tu ya kujipata katika mgogoro huo wa kisheria kwa kosa la kupiga kelele.

Aliyeshtaki anasema kuwa Bi Fesseau alianza kubisha baada ya kupewa taarifa za kelele zilzosababishwa na jogoo wake na kusababisha mgogoro

Aidha wafuasi wanaomuunga mkono Bi Fesseau wanasema kwamba jogoo huyo ni sehemu ya maisha ya watu wa vijijini hivyo hawezi kunyamazishwa

Mahakama ilitegemea kutoa uamuzi wake mwezi Septemba. Mwaka 2019 mahakama ilimpendelea Jogoo Maurice na kuamuru aishi katika visiwa vya Oleron.

Jogoo huyo alikufa Mei lakini mmiliki wake Bi Fesseau alisubiri muda muafaka kutangaza kifo chake “nilijiambia kwamba kwasababu ya hatua ya kutotoka nje na watu wana mambo mengi ya kukabiliana nayo” alisema Bi Fesseau

“Tumenunua Jogoo mpya na huyo pia tumemuita Maurice, naye pia anawika kama yule wa kwanza lakini hawezi kuwa Maurice wetu” aliongeza Bi Fesseau

Walalamishi Jean Louis Biron na Joelle Andrieux walijenga nyumba yao katika kijiji cha Pierre de Oleran ambalo pia ni eneo la kitalii karibia miaka 15 iliyopita pia wanasema kuwa moja kati ya sababu iliyowapelekea wao kujenga nyumba eneo hilo ni utulivu wa eneo hilo.

lakini mambo yalianza kubadilika 2017 pale Jogoo Maurice alipoanza kuwika kila mara tena kwa sauti ya juu mno.

Septemba mwaka jana Jaji alitoa uamuzi unaompendelea Jogoo Maurice kwa kuamuru aliyeshtaki kulipa Pauni 1000 sawa na (Euro 900, USD 1,100) kama fidia.