Kampuni ya mtandao wa kijamii wa Facebook hivi karibuni imeondoa matangazo ya kampeni ya Rais Donald Trump baada ya kutumia alama zilizokuwa za utawala wa kinazi wa Ujerumani

Facebook imesema kuwa alama ambayo ililengwa kuondolewa ni alama ya pembe tatu nyekundu kama ilivyokuwa ikitumika katika utawala wa kinazi nchini Ujerumani kuwatambua wapinzani wao kama ni wakomunisti.

Alama hiyo ni sehemu ya matangazo ya kampeni ya Trump kwa uchaguzi mkuu nchini Marekani mwaka huu

Hata hivyo timu ya kampeni ya Trump imekanusha na kusema kuwa tangazo hilo lilikuwa likilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto antifa amabcho wanadai wanatumia nembo hiyo

Aidha Facebook imeeleza kuwa “haturuhusu alama ambazo zinasimama kwa mirengo ama maudhui ya chuki, labda iwe yenye kukemea jambo hilo”

Mkuu wa sera za ulinzi Facebook Nathanie Gleicher ameeleza kuwa “hiko ndicho tulichokiona kwenye tangzo hili, na popote ale alama hiyo itakapotumika tutachukua hatua kama hii”

Matangazo hayo yalipakiwa kwenye kurasa za mtandao wa Facebook za Trump pia makamu wake Mike Pence kisha zikaondolewa ndani ya saa 24