MKONGWE wa muziki wa bongo fleva Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego hivi karibuni ameweka wazi kuhusiana na shinikizo analopata kutoka kwa mama yake kuhusu kuondoa video ya ngoma yake mpya inayotamba kwa jina la “Mungu yuko wapi?” katika mtando wa YouTube.

Nguli huyo ameweka video iliyobeba ujumbe huo katika ukurasa wake wa instagram akiwashukuru mashabiki wake kwa jinsi walivyopokea vizuri nyimbo hiyo, lakini pia akazungumzia kuhusiana na shinikizo analopata kutoka kwa mama yake kuiondoa video hiyo isiendelee kutazamwa.

Mpaka hivi sasa bado mama wa msanii huyo hajaweka wazi kwanini hasa amemuambia mwanaye afute video hiyo kutoka katika mtandao wa youtube “bimkubwa anasema nifute video ya Mungu yuko wapi, hajanipa sababu kasema tu nifute” ameandika Nay

BOFYA HAPA KUTAZAMA PICHA ZA NAY