MSANII wa muziki kutoka nchini Tanzania anayetamba kwa albamu ya Afro East maarufu kama Harmonize, hivi leo ameeleza hisia zake kupitia katika ukurasa wake wa instagram.

Harmonize ameandika kuwa “ilikuwa ndoto yangu ya siku nyingi kufanya kazi na dada yangu kipenzi Lady Jay Dee, niamini mimi ni shabiki yake mkubwa sana nimeanza kumsikiliza na kumuona tangu nikiwa mtoto na mwishowe ndoto zangu zimetimia”

Msanii huyo ameyatoa ya moyoni mwake baada ya kuachia video ya ngoma yake ya wife ambayo amemshirikisha mwanadada huyo mkongwe katika mziki wa bongo fleva.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA VIDEO MPYA #HARMONIZE