IKIWA imebaki miezi michache kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, baadhi ya wanasiasa wameweka wazi nia zao za kutaka kuwania nafasi katika kiti cha Urais kupitia vyama mbalimbali.

Siku ya jana Mbunge wa Iringa mjini kupitia CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu 2020 kupitia chama cha CHADEMA.

Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa “kama nilivyotangaza siku chache zilizopita leo ninatangaza tena ni yangu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria na taratibu za CHADEMA tayari nimewasilisha taarifa rasmi ya nia yangu ya kugombea”

“kwanini ninautaka Urais? nataka kuongoza mageuzi makubwa ya kiutawala, kiuchumi na kielimu, yatakayoleta maendeleo makubwa endelevu na ya haraka yenye manufaa kwa sasa na Tanzania ijayo” aliongeza Msigwa

Mpaka kufikia hivi sasa Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu ndiyo viongozi wa chama hicho ambao tayari wamewasilsha taarifa zao rasmi zenye nia ya kugombea urais 2020 kupitia chama hicho

Kauli ya Nyalandu anasema kwamba “Endapo chama changu kitaniteua kugombea na Watanzania wakanipa ridhaa kuwaongoza, nitasimamia mambo yafuatayo ndani ya siku 100, kwanza nitaunda maridhiano ya kitaifa ili kuwaunganisha watu wote, Jambo la tutaandaa mpango wa kufuta sheria zote kandamizi zinzosababisha watu kuwekwa kizuizini bila dhamana yoyote kisha tutawatoa gerezani watu wote ambao wamewekwa bila ya kuwepo na due process”

Pia niataongeza ajira kwa vijana na jambo lingine ndani ya siku mia moja nitaanza upya mchakato wa mapitio ya katiba kuanzia ile ya jaji warioba na jambo la sita tutairekebisha TRA ili iwe taasisi isiyolalamikiwa kwa namna yoyote ile” aliongeza Nyalandu

Aidha kwa upande wa Tundu Lissu amesema kuwa “Kwa kipindi cha miaka mitano itakayoishia oktoba mwaka huu nchi yetu imetawaliwa na serikali ya Rais John Pombe na Chama Cha Mapinduzi kwa namna ambayo imeiweka serikali yetu katika mtihani mkubwa kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia, kwa mtihani huu nchi yetu iko njia panda na kwa vyovyote vile itakavyokuwa uchaguzi huu lazima utakuwa na historia kubwa kwa nchi yetu”