MAUAJI ya mtu mweusi mwingine wakati maandamano yakiwa yanaendelea nchini Marekani yamesababisha shutuma mpya za utumiaji wa nguvu kupita kiasi.

Rayshard Brooks, 27, alipigwa risasi siku ya ijumaa akiwa katika mgahawa ambao ni maarufu kwa jina la Wendy’s na kwa sasa mgahawa huo umechomwa moto.

Waandamanaji huko Atlanta waliandamana wikiendi hii ili kushinikiza kuchukuliwa kwa hatua na mamlaka dhidi ya mauaji ya bwana Brooks.

Idara ya uchunguzi ya Georgia inafanya uchunguzi juu ya mauaji ya Rayshard Brooks, inatafuta video za kamera za usalama pamoja na picha za mashuhuda ndani ya mgahawa wa Wendy’s

Moja kati ya video zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo inamuonesha Bwana Brooks akiwa anapambana na polisi hao wawili nje ya mgahawa huo.

Bwana Brooks alifanikiwa kukamata silaha ya polisi na kukimbia nayo lakini polisi mwingine alifanikiwa kumnasa kwa kutumia silaha ya umeme, kisha walitoweka kwenye video hiyo.

Milio ya risasi ikasikika na baada ya sekunde chache Bwana Brooks alionekana akiwa amelala chini, alipelekwa hospitali lakini baadae alipoteza maisha mmoja wa polisi alitibiwa majeraha aliyoyapata katika tukio hilo

Taarifa kutoka ofisi ya mwanasheria wa kaunti ya Fulton imesema inafanya uchunguzi juu ya tuko hilo