HABARI

Tundu Lissu aweka wazi nia yake ya kugombea Urais Tanzania

MWANASIASA wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, hii leo ameweka wazi nia yake ya kuwania urais kupitia chama chake cha CHADEMA

Akizungumza kutokea ughaibuni ambako alipelekwa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Lissu ameeleza nia yake ya kuwania nafasi ya urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu

“sasa ninapenda kuwataarifu rasmi kwamba nimetangaza rasmi nia yangu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Tayari nimeshawasilisha taarifa rasmi ya kutangaza nia hiyo kwa katibu mkuu wa chama chetu kama ilivyoelekezwa kwenye maelekezo yake kwa wanachama wa chama chetu”

Akiongea mubashara kupitia mitandao ya kijamii, mpinzani huyo wa serikali amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia kuwa endapo atafanikiwa kukalia kiti cha Urais wa Tanzania hatoruhusu serikali yake kulipiza kisasi.

Ikumbukwe kuwa tangu awali Lissu amekuwa mmoja kati ya wakosoaji wakubwa wa serikali ya Rais John Pombe na hivyo hata kwenye hotuba yake leo ameendelea kukosoa baadhi ya mambo ambayo anayaona kuwa hayapo sawa katika serikali ya Rais John Pombe.

Click this link to create a WordPress website and earn from AdWord and GoogleAds – WordPress Website

“Kwa kipindi cha miaka mitano itakayoishia oktoba mwaka huu nchi yetu imetawaliwa na serikali ya Rais John Pombe na Chama Cha Mapinduzi kwa namna ambayo imeiweka serikali yetu katika mtihani mkubwa kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia, kwa mtihani huu nchi yetu iko njia panda na kwa vyovyote vile itakavyokuwa uchaguzi huu lazima utakuwa na historia kubwa kwa nchi yetu”

Aidha Lissu ameweka ahadi kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais basi serikali yakeitaandaa sera thabiti za kiuchumi ambazo zitahakikisha kuwa serikali yake inabaki kuwa mwangalizi za kiuchumi zinazoendeshwa na sekta binafsi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.