HIVI karibuni mataifa mengi duniani yamelegeza sheria ambazo zilikuwa zikilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya corona, huku mataifa mengine yakiondoa lockdown na kuruhusu wanafunzi kurudi shuleni kuendelea na masomo kama ilivyokuwa hapo awali.

Ijapokuwa kumekuwepo na baadhi ya sheria na utaratibu ambao umewekwa ili kuendelea kuzuia maambukizi ya virusi vya corona bado Shirika la Afya duniani linaeleza juu ya uwezekano wa kuwepo kwa maambukizi mapya ya virusi vya corona.

Hivi majuzi Mwanabailojia Dkt Jennifer Rohn ambaye amekuwa akifuatilia vile janga la corona linavyoendelea huko Asia na kusambaa duniani kote alisema kuwa “Mlipuko wa pili wa janga la corona sio tena suala la ikiwa inaweza kutokea badala yake ni lini itatokea na athari yake itakuwaje”.

Maneno ya Dkt Jennifer Rohn yanasindikizwa na kauli iliyotolewa na WHO inayosisitiza kuwa ” maambukizi mapya huenda yakaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu zaidi hivyo tunahitaji juhudi za pamoja hili kuudhibiti”

China ilikuwa nchi ya kwanza kupata janga la corona na kurekodi data muhimu

MAISHA BAADA YA KUTOKA KIZUIZINI…

Dkt Jennifer Rohn anasema kuwa “maambukizi huja wakati wa kuondoa vizuizi, hiki ndicho kinachofanyika unapokuwa na virusi vipya ukiwa hakuna kinga mikononi mwa watu” baada ya vizuizi kulegezwa zimekuwepo tabia hatarishi ambazo huweza madhara makubwa na kusababisha maambukizi endelevu ya ugonjwa huu.

Mtindo wa maisha ambao tuliishi awali kabla ya ujio wa corona ndio huohuo unaoweza kuleta maambukizi mapya ya ugonjwa huu, kupigana mabusu, kukumbatiana mikusanyiko isiyo na lazima pamoja na kazi (haimaanishai kuwa tusifanye kazi) ambazo tulikuwa tukizifanya hapo awali huweza kuwa kipaumbele katika kueneza ugonjwa huu.

Historia inaeleza kuwa milipuko ya pili ni kawaida katika ya majanga ya magonjwa ya kuambukiza mfano SARS ambapo maambukizi yaliendelea kuwepo mara baada ya kulegezwa kwa masharti na watu kurudia katika hali ya kawaida.

Hivyo tunaona kuwa ni vigumu kwetu kuepukana na mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona kama Shirika la Afya duniani linavyoonya na kulekeza mambo ya muhimu kufuata katika kukabiliana na ugonjwa huu

corona virus measures in africa

Aidha uwezo wa kupambana na ugonjwa huu unategemea umoja tulionao, usikivu na juhudi binafsi katika kumlinda umpendae au yeyote aliye karibu nawe kwa kufuata utaratibu ambao serikali ya taifa husika imejipangia.