sehemu ya 01

Simu yangu ya mkononi iliita na jina ilionesha mama kuwa ndiye aliyekuwa akipiga, niliharakisha kuipokea kwani ni muda mrefu ulikuwa umepita sikumuona mama yangu.

Nakumbuka ni miaka miwili imepita tangu nilipoondoka nyumbani, nami nilikuwa barabarani kurejea baada ya kupigiwa simu na jirani yangu kuwa mama yangu anaumwa sana.

Niliipokea simu ile huku moyo wangu ukiwa umejawa hofu na maswali tele, ghafla niliisikia sauti ya kike nilitambua haikuwa ya mama yangu, nilitega sikio makini kuisikiliza.

“Hallo…. Wewe ni Suzana….?”  sauti hile iliuliza ikiwa imejawa na jazba nilihisi kuwa huenda hali ya mama yangu itakuwa mbaya sana nami nilihitajika haraka sana.

“Ndiyo…. Ndiyo ni mimi Suzana…” nilijibu bila kuchelewa.

Niliwaeleza kuwa niko njiani, nakaribia kufika hivyo wasiwe na wasiwasi sana…

Yapata saa moja na nusu majira ya usiku niliwasili kijijini kwetu Bumbuta kwa kuwa bado nyumba hazikuwa zimebadilika sana basi nilijitahidi kubahatisha mpaka nikafika nyumbani.

Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio, baada ya kukuta watu wengi akili yangu ilianza kuhisi kuwa huenda mama yangu kipenzi ameshapoteza maisha, nilipiga moyo konde huku machozi yakinilenga, nilijikaza kisabuni na kupiga hatua zangu kuelekea chumbani alikolazwa mama yangu.

Nilipofika ndani niliona wanawake watatu wakiwa wamezingira kitanda alicholalia mama yangu, hao niliweza kuwatambua kuwa ni majirani baada ya kuangalia nyuso zao.

Wakati huo mama yangu alikuwa akinitizama usoni, majirani wale walinipisha ili niongee na mama yangu, sikuamini kuwa mama yangu ni mzima hadi pale nilipoisikia sauti yake kwa mara ya kwanza

“Uu—jaaa–mbo mwana–ngu kipensi Su—zana?” mama aliniuliza kwa upole.

“Sijambo mama yangu hali yako ni mbaya sana mama… ni vema tuende hospitali.”….

Mama yangu hakujibu kitu chochote tena niliinuka haraka kisha nikawaomba majirani wanisaidie tumpeleke mama hospitali.

Usiku uleule bila kusubiri tuliita usafiri kisha tukampleleka mama hospitali, alipofika hospitali alichukuliwa na wauguzi kisha akaanza kupatiwa huduma kama mgonjwa wa dharura, kusema ukweli hali ya mama yangu ilikuwa inatia wasiwasi, muda wote nilitamani kutoa machozi lakini nilijizuia kufanya hivyo.

Penzi la wakala wa Giza; Ep 01

Penzi la wakala wa Giza; Ep 02.

Tulikaa nje ya chumba hicho tukisubiri majibu ya ugonjwa wa mama yangu kutoka kwa daktari, ghafla Daktari alikuja kisha akauliza ni yupi kati yetu anaitwa Suzana. Nikasimama na kutoa ishara kuwa ndiye mimi basi akanambia mama yako anakuhitaji ndani, nilishangazwa kwanini mama anihitaji wakati wa kupatiwa matibabu ya dharura?. Nilipiga hatua mbele huku nikiusikia moyo wangu kuwa ni wabaridi mno.

Nilitembea kwa haraka mpaka ndani, mama yangu alipoiona sura yangu alitabasamu kisha akanishika mkono na kuniambia.

“Suzana mwanangu… wewe ni mwanangu nikupendaee, naomba uwe jasiri mwanangu kuyaendesha ma—isha yako mwenyewe.” Mama yangu aliniambia.

“Uhai wangu umef—ika ukingoni mwanangu, pumzi yangu huwezi kuik—omboa mwanangu lakini nisikilize kwa makini sana” mama yangu aliendelea kunisihi..

Mama yangu aliongea kwa shida lakini nilimuelewa hapo macho yangu yalikuwa yanabubujikwa na machozi, aliendelea kunipa maelekezo ndipo akaniambia kuwa chini ya kitanda chake ameweka kisanduku chenye majibu ya kila kitu ambacho nilikuwa nikimuuliza siku zote bila kupata majibu.

“mwanangu Suzana mwanzo wetu mimi na baba yako ulikuwa mgumu sana— hakikisha una ujasir….i wa kutosha ndipo uweze kuki– fungua kisa…nduku hiko” mama yangu alinisisitiza.

Nilimwambia mama yangu huu si wakati wa kukumbuka maswali na malalamiko yangu hapo awali, bali ni muda wa kumuombea ili apoone tuwe wote pamoja.

Maombi yangu hayakufua dafu, mama yangu alikata roho baada ya kusema maneno yale, moyo wangu uliuma sana nililia kwa uchungu majirani wengi walifika kunibembeleza lakini haikusaidia kitu, nililalama kuwa nguzo yangu imeondoka duniani nilitamani hata kukufuru jina la mwenyezi Mungu kwanini amchukue mama yangu mapema vile.

Msiba ulirudishwa nyumbani na taratibu zote za mazishi zikafuata, mama yangu akazikwa huku macho yangu yakishuhudia mambo yote hayo, moyo wangu ulikuwa baridi kama vile umegandishwa kwa barafu, akili yangu ilimuwaza mama yangu muda wote.

Siku tatu za mazishi zilishapita na watu tayari walishaanza kupungua nyumbani kwetu nilibaki mwenyewe tu ndipo nikaona ni wakati muafaka wa kufungua kile kisanduku ambacho mama yangu alinieleza.

Nilikitoa uvunguni ambako mama yangu alikiweka, nilikiangalia kwa muda, nilitamani kujua ndani yake kuna nini ila nilighairi kukifungua kwa muda ule, nikaamua kukiweka kwenye begi langu la safari huku nikijiapiza kuwa ningekifungua nikiwa safarini.

Asubuhi na mapema nilidamka na kujiandaa ili nianze safari ya kurudi mjini kuendelea na safari yangu ya kutafuta maisha, moyo wangu ulikuwa umejawa na masononeko, akili yangu ilijawa na huzuni kubwa niliwaza imekuwaje mpaka kaka yangu wa tumbo moja hakuweza kuhudhuria katika msiba wa mama yetu?, alikuwa wapi kaka yangu je ni dhahiri kuwa kaka yangu hakupata taarifa za msiba?.

Jambo lililoniumiza zaidi ni kwamba mama yangu hakuwa anapenda kuzungumza jambo lolote kuhusu kaka yangu siku zote aliniambia tu kuwa nina kaka na ipo siku nitamuona, hakuwahi hata kunitambulisha kwa kaka yangu japo alinambia kuwa kaka yangu ananifahamu kwa jina tu.

Nilikumbuka siku moja jioni kabla sijaondoka kuelekea mjini nilikuwa nimekaa na mama yangu nikimenya mihogo nilijaribu kumuomba anisimulie jinsi kaka yangu alivyo na kwanini tumetenganishwa.

Mama yangu alikasirika sana, na ghafla tu machozi yalianza kumtoka kisha akaniambia “kaka yako ni mtu mwema sana, tena mstaarabu na mzuri pia, aliondoka nyumbani hali wewe ungali mdogo, mwanangu alituacha ungali mdogo sana lakini haya yote ni baba yako aaah!!.”

Processing…
Success! You're on the list.

Alilia kwa uchungu sana mama yangu hata nikamuonea huruma, nikahisi ndio sababu hataka hata mimi nimjue kaka yangu lakini nilibaki na swali moja jioni hile, kwanini baba yangu, yeye alimfanya nini mama yangu sikuwahi kufahamu hili kabisa.

Siku hile niliazimia kuondoka na kurudi mjini kuendelea na maisha yangu japo ni wiki chache zilikuwa zimepita baada ya kumzika mama yangu kipenzi Bi Sauda nilikusanya kila kitu ambacho ningehitaji katika safari yangu, sikusahau kisanduku kile ambacho niliona kama kimebeba historia ya familia yangu.

Niliamua kukiweka ndani ya mkoba wangu wa mkononi kisha nikafunga mlango nikabeba mabegi yangu na kutoka nje.

Nilimuita jirani yetu ambaye alinisaidia sana katika shughuli zote za msiba, licha ya hivyo yeye ndiye ambaye alikuwa karibu na mama yangu pale ambapo mimi sikuwepo, nilimkabidhi funguo za nyumbani na kumuomba anisaidie kuiangalia nyumba yetu mpaka pale nitakaporudi.

“Suzana unakwenda wapi binti yangu ni siku chache tu tangu mama yako atutoke” alisema kwa unyonge
“Usihofu mama yangu nakwenda kutafuta maisha lakini nitarudi usijali mama yangu” nilimjibu kwa upole sana kwani alikuwa mama wa makamu tena mwenye upendo nami.

Basi aliniruhusu nami nikamuachia nyumba na kuanza safari yangu, nilitazama akiba niliyokuwa nayo mfuko niliona kuwa nina fedha taslimu Shilingi laki sita niliamini kuwa hizi zingeweza kunifikisha mjini Dar es salaam bila shida yoyote.

Itaendelea…