MSANII wa muziki wa kufoka kutoka Tanzania Roma ambaye kwa sasa anashirikiana na Stamina katika kundi lao kama “Rostam” hivi karibuni amekuwa akiweka wazi baadhi ya siri ambazo zimejificha katika video ya nyimbo yao mpya iliyoenda kwa jina la “KAKA TUCHATI”

Siku moja iliyopita Roma aliweka wazi mchakato mzima uliopelekea kupatikana kwa kiitikio cha nyimbo hiyo, lakini hivi leo Roma ameweka video nyingine katika ukurasa wake wa instagram na kutoa siri nyingine tena.

Katika video hiyo Roma ameeleza kuwa mpenzi wa Stamina alikuwa amevaa nguo nyekundu akiwakilisha wachezaji na mashabiki wote wa timu ya mpira wa miguu ya Simba, huku Stamina mwenyewe akiwa amevaa jezi ya njano kama mshabiki wa klabu ya Yanga.

Pia mpenzi wa Stamina alionyeshwa akiwa na mimba, kwa tafsiri ya Roma alisema kuwa “Stamina anamaanisha kawatia mimba simba wote, wachezaji, mashabiki, wapenzi na watu wote ambao ni timu Simba”