Rais wa Marekani The real Donald Trump hivi karibuni ametembelea kiwanda cha Honeywell cha kutengeneza barakoa, na kustaajabisha wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya kukataa kuvaa barakoa ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa covid-19.

Akiwa anaelekea kuingia ndani ya kiwanda hicho kilichopo katika jimbo la Arizona, mlangoni alikuta onyo lililosomeka kuwa “vaa barakoa yako muda wote” licha ya kuliona onyo hilo Donald Trump hakujali na aliingia ndani ya kiwanda hicho bila kuvaa barakoa.

Hali hii inaonesha kuwa Rais Trump amekataa katakata kuvaa barakoa licha ya yeye mwenyewe kuunga mkono hoja ya wananchi wa Marekani kuvaa barakoa, Aprili 3, 2020 Bwana Trump alisema kuwa angalau anaweza kuvaa barakoa iliyotengenezwa kwa kushonwa nguo au kitambaa.

“Sidhani kama nitavaa hivyo, kuvaa barakoa usoni huku nikiwa nawasalimia Marais wenzangu, mawaziri, madikteta, wafalme na malkia siwezi kabisa…. sidhani labda huko mbeleni nitabadilisha mawazo yangu” alisema Donald Trump