NYOTA wa muziki kutoka Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa makampuni yaliyo chini ya lebo ya Wasafi (WCB) Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz amempongeza mwanamuziki Zuchu, kwa kuingia katika kumi bora ya wasanii kutoka Tanzania wanaoongoza kwa kazi zao kutazamwa katika mtandao wa Youtube.

Pongezi zake zimefuatiwa baada ya tovuti ya Swahili Times kutoa orodha yenye majina kumi ya wasanii ambao kazi zao zimetazamwa mara nyingi katika mtandao wa youtube kwa mwezi Aprili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram nguli huyo ameweka wazi jinsi alivyopendezwa na uchapaji kazi wa mwanadada huyo, huku akiwasifu wanawake wenzake kwa kumuunga mkono katika kuusikiliza na kuusambaza muziki wake.

Zuchu ni mmoja kati ya wasanii chipukizi ambao kwa sasa wamejiunga na lebo ya WCB ambayo ipo chini ya usimamizi wa Diamond Platnumz,