HABARI

Watu ‘bilioni moja’ huenda wakaambukizwa virusi vya corona duniani kote

Shirika la Kutoa Misaada la Kimataifa (ICRC) limesema kuwa katika siku zijazo huenda maambukizi ya virusi vya corona yakafikia watu bilioni moja,

Shirika hilo linalojihusisha na utoaji wa misaada limeona kuwa utoaji wa huduma za kibinadamu pamoja na fedha unahitajika zaidi ili kupunguza kasi ya usambaaji wa virusi hivyo.

ICRC pia imeonya kuwa muda uliobaki kuimarisha hali ni mchache mno hivyo nchi zenye vita mara kwa mara kama Afghanistan na Syria zinahitaji msaada wa dhartura wa kifedha ili kusaidia kuzuia mlipuko wa virusi vya corona.

Hadi kufikia sasa dunia inashuhudia takribani watu milioni tatu wakiwa tayri wameambukizwa ugonjwa huu, huku vifo zaidi ya 200,000 vikithibitishwa kulingana na takwimu za chuo cha Johns Hopkins, Marekani

Awali ripoti ya shirika hilo ambalo pia inazingatia data kutoka Shirika la Afya Duniani na WHO na Chuo Cha Imperial College London zilisema kuwa maambukizi yanaweza kufikia watu milioni 500 mpaka bilioni 1. Huku idadi ya vifo ikiwa imekadiriwa kufikia watu milioni tatu kwa nchi zinzkumbwa na migogoro na zisizokuwa na uthabiti.

“Idadi hiyo inafaa kutufumbua macho” amesema mkuu wa Shirika la ICRC, David Miliband.

“Maafa ya janga ili bado hayajashuhudiwa sana katika nchi zilizokumbwa na vita hivyo ni muhimu sana wafadhili kutenga fedha kwa ajili ya nchi zilizokumbwa na vita” aliongeza Bwana David.

Aidha Caroline Seguin, anayesimamia miradi ya matibabu nchini Yemen kupitia shirika la Matibabu lisilokuwa na mipaka amesema kuwa Shirika hilo linaamini kuwa raia wengi wamekufa kwa ugonjwa wa covid 19 ingawa sio hospitalini.

Akiliambia shirika la BBC alisema kuwa “tunaamini kuwa maambukizi ya ndani kwa ndani bado yanaendelea ingawa watu wanaopimwa ni wachache “

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.