MSANII wa muziki wa kufoka kutoka Tanzania, Rosary Robert almaarufu kama Rosa Ree amerejea tena na kusema maneno machache ikiwa ni kama utangulizi kabla ya kuachia ngoma yake ya Sukuma ndinga remix.

Ngoma hiyo aliyoshirikiana na Rayvanny mmoja kati ya waimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka katika kundi la WCB, Rosa amesema kuwa sukuma ndinga remix itakuwa zaidi ya movie.

Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram, “Haina haja ya Netflix, tupo tayari kuwapa nyote filamu sukuma ndinga remix mkoo tayari”.