RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongelea sakata la uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 3 mwezi Novemba mwaka huu

Akizungumza katika hotuba yake kutokea White House Rais Trump amekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa kubadilisha tarehe ya kufanya uchaguzi huo kufuatiwa na kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona.

Akiwa anazungumza katika hotuba hiyo Trump aliulizwa swali kama ana mpango wowote wa kubadilisha tarehe ya uchaguzi,

“sikuwahi hata kufikiri kubadilisha tarehe ya uchaguzi” rais Trump alijibu “Kwanini nifanye hivyo? Novemba 3 hiyo ni namba nzuri” alimalizia.

Pia makamu wa rais mstaafu, Joe Biden aliliambia shirika la utangazaji BBC kuwa kutokana na hali jinsi inavyokwenda aliwaza kuwa rais Trump angeweza kubadilisha tarehe ya uchaguzi.

“hatuna furaha na china”

Aidha akiwa katika hotuba yake Rais Trump amedhihirisha kuwa Marekani haina furaha na nchi ya China kufuatiwa na uchunguzi uliofanywa juu ya kusambaa kwa virusi vya corona duniani kote.

“na hatuna furaha na China, hatuna furaha na hali yote, kwani tunaamini ingeliweza kuzuiwa katika chanzo chake, ingezuiliwa kwa haraka na isingesambaa duniani kote” Trump alisema.

Katika madai yake Trump anasema kuwa hakuna nchi inayoweza kuwajibishwa kwa kosa la kusambaa kwa virusi vya corona isipokuwa China.

“Hakuna anayemlaumu mwenzake hapa isipokuwa tunaagalia nani angeliweza kuzuia maambukizi angali bado yakiwa changa, Wao (akimaanisha China) wangeliweza kuikinga dunia dhidi ya janga hili”, alisema Trump

Chapisho liliwekwa na BBC News katika mtandao wa Tweeter likimuonesha Rais Trump akiwa anahutubia White House