Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC ) nchini Marekani vimetangaza ongezeko la dalili mpya sita zitokanazo na maambukizi ya ugonjwa wa corona

Siku ya jumapili CDC waliongeza dalili mpya ambazo mgonjwa aliyepata maambukizi ya virusi vya corona anaweza kuzisikia, dalili hizo ni; Mgonjwa kuhisi baridi kali, Kutetemeka mara kwa mara na baridi, maumivu ya misuli, homa, kukohoa, na mgonjwa kupata ugumu katika mfumo wa upumuaji.

Aidha CDC wamesema kuwa dalili hizo zinaweza kujitokeza ndani ya siku mbili hadi 14 baada ya mgonjwa kupata maambukizi ya virusi hivi.

Processing…
Success! You're on the list.