HABARI

Taylor Swift aghairisha matamasha yote 2020 ‘asema hilo ndilo chaguo sahihi’

NYOTA wa muziki Pop kutoka Marekani Taylor Swift, ameamua kughairisha maonyesho yote aliyotakiwa kufanya ndani ya mwaka 2020 ili kuunga mkono kauli mbiu ya “kaa nyumbani kaa salama”.

Mwanamama huyo anayetamba kwa albamu ya Lover aliyoiachia mwishoni mwa mwaka 2019 alitakiwa kuzunguka maeneno mbalimbali kama Marekani, Ulaya na Amerika ya Kusini ili kuitangaza albamu hiyo.

Lakini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona ametakiwa kutupilia mbali ziara yake katika mataifa hayo huku akiweka ahadi kuwa ziara hiyo yaweza kufanyika mwaka 2021 endapo mambo yatakuwa shwari.

Swift ameandika katika ukurasa wake wa twitter “nina huzuni kubwa, hatutoweza kuonana tena katika matamasha kwa mwaka huu lakini natambua haya ndiyo maamuzi sahihi”

“Tafadhali, tafadhali baki na afya njema, kaa salama tutakuwa pamoja katika tamasha mapema iwezekanavyo, kilicho muhimu kwa sasa ni kubaki karantini” aliongeza Taylor.

Kwa mujibu wa ratiba iliyoweka na uongozi wa Swift, matamasha yaliyotakiwa kufanywa Marekani pamoja na Brazil yamesogezwa mpaka 2021, tarehe itatangazwa na Taylor mwenyewe.

1 reply »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.