Baada ya mlipuko wa ugonjwa wa corona ligi zote za ulaya zilisitishwa kama hatua mojawapo ya kupunguza mkusanyiko wa watu ili kuzuia kasi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Mpaka sasa kwa baadhi ya nchi za Ulaya hali ya maambukizi inaonekana kufika kileleni kutokana na kupungua kwa idadi ya vifo na maambukizi yanayotokea kwa siku.

ipi ni hatima ya ligi hizo?

Majadiliano yaliyofanywa siku ya ijumaa na klabu zinazoshiriki katika ligi ya Premia , imeamriwa kuwa ligi hiyo itaendelea ili kukamilisha mechi 92 zilizosalia, ijapokuwa ligi hiyo haijapanga bado tarehe rasmi ya kurudi uwanjani.

“Pamoja na biashara nyingine na viwanda ligi ya premia na vilabu vyetu tunapanga mipango migumu inayoweza kutokea” ilisema ligi hiyo

Mpaka kufikia sasa ligi ya Ujerumani ya Bundesliga, klabu zimerudi mazoezini lakini msimu umeahirishwa hadi Aprili.

Aidha LaLiga ya Uhispania imetangaza kutokuwa na mazoezi mpaka pale harakati za dharura zilizowekwa na rais wa ligi hiyo Javier Tebas kuondolewa

Pia Ligi 1 ya Ufaransa, mamlaka ya soka nchini humo imefikiria kuanzisha ligi hiyo ifikapo tarehe 3 au 17 mwezi Juni

Serie A ya Italia nayo inataraji kuanza kuwapima wachezaji wake mwanzo wa mwezi Mei ili kuendelea na ligi hiyo.

Processing…
Success! You're on the list.