MWANAMUZIKI Beyonce Knowles kutoka Marekani, amewastaajabisha mashabiki wake baada ya kuimba nyimbo kwa ajili ya wafanyakazi wa afya katika tukio la kuimba nyimbo za pamoja maarufu kama Singalong iliyofanywa na kampuni ya uandaaji filamu ya Disney.

Mama huyo wa watoto watatu ameimba nyimbo hiyo akiwa nyumbani kwake ikiwa kama sehemu ya maagizo yanayolenga kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Processing…
Success! You're on the list.

Maudhui yaliyomo ndani ya nyimbo hiyo iliyokwenda kwa jina la When you wish upon a star yamelenga kuwashukuru wafanyakazi walioko mstari wa mbele kupambana dhidi ya ugonjwa wa corona.

“Ninapenda kuutoa wimbo huu kwa wafanyakazi wote wa mashirika ya afya waliofanya kazi bila kuchoka ili kutuweka katika hali ya usalama, ninathamini mchango wenu” alisema Beyonce

Baada ya kumaliza kuimba wimbo huo, nyota huyo alimalizia kuwa kutoa rai yake kwa familia zilizoko nyumbani “Tafadhali mushikamane katika familia zenu, mukae salama bila kukata tamaa naahidi tutalishinda hili” aliongeza Beyonce.

Ikumbukwe kuwa Beyonce ameanza kuwa mwanafamilia wa kampuni za Disney baada ya kushiriki katika utengenezaji wa filamu ya The Lion King ya mwaka 2019 akiingiza sauti kama Nala.