WAKENYA waliokuwa kwenye karantini ya lazima wafanya mgomo na kutishia kutoroka katika kituo hicho kilichopo mjini mkuu wa Nairobi.

Sababu zilizopelekea kuwepo kwa mgomo huo ni kwamba Wakenya hao wanadai kuwa si haki kuendelea kubaki karantini huku wakiwa wamefanyiwa vipimo mara mbili na kutokutwa na maambukizi vya virusi hivyo.

Juma lililopita serikali ya Kenya ilitangaza ongezeko la muda wa kusalia karantini kutoka majuma mawili mpaka kufikia mwezi mmoja baada ya kupatikana wakikaidi baadhi ya maagizo ya serikali hiyo katika vita dhidi ya maambukizi ya corona.

Japo walioko karantini wanasema kuwa kuongezwa kwa muda huo kunawafanya kuugua shinikizo la akili.

Watu wawili wamekutwa na virusi vya corona kati ya watu 21 waliowekwa karantini katika Chuo Kikuu cha Kenya (KU), watu hao wawili wanakamilisha idadi ya watu tisa ambao wametangazwa na serikali ya Kenya hivi leo na kufanya idadi kamili 225 ya watu walioathiriwa na virusi vya corona nchini humo.

Kutokana na ripoti ya Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema kuwa maambukizi hayo mapya yaliripotiwa baada ya sampuli 803 kufanyiwa vipimo ndani ya saa 24 zilizopita.

Processing…
Success! You're on the list.