JITIHADA zilizowekwa na Shirika la Afya duniani WHO zakosolewa vikali na Rais Trump huku akidai kuwa Marekani itasitisha ufadhili wake wa Dola Milioni 400 kwa shirika hilo

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa uongozi wake utasitisha ufadhili kwa Shirika la Afya duniani (WHO) kwa madai kuwa WHO imeshindwa kufanya majukumu yake muhimu ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona duniani.

Pia rais Trump ameishutumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kukabiliana ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vilianzia China.

Hapo awali Bwana Trump aliishutumu WHO kwa kuipendelea China

“Ninawapa muongozo utawala wangu kusitisha ufadhili wakati shirika la afya la duniani likiwa linachunguzwa katika majukumu yake iliyoshindwa kuyatimiza katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona” Rais Trump aliwaambia waandishi wake katika White House.

Rais Trump ameishutumu WHO kwa kushindwa kukabiliana na ugonjwa huu tangu ulipoanza kwa mara ya kwanza mjini Wuhan

Japo hivi karibuni Bwana Trump aliandika katika ukurasa wake wa twitter akiisifu China kwa jitihada walizochukua katika kukabiliana na ugonjwa huu

Aidha rais Trump aliongeza kwa kusema kuwa Shirika la Afya duniani limeshindwa kutimiza majukumu yake muhimu na wanapaswa kuwajibishwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisema kuwa wakati huu si wa kukata ufadhili kwa WHO

Marekani ndiye mfadhili mkubwa kwa shirika hilo, anachangia asilimia 15 ya bajeti ambayo ni sawa na dola milioni 400, huku shirika hilo likitenga kiasi cha dola milioni 675 ili kukabiliana na janga la corona japo imeripotiwa kuwa shirika linaweza kuongeza bajeti mpaka karibia dola bilioni moja.

sababu za KUKOSOLEWA KWA SHIRIKA LA AFYA duniani (WHO)

Processing…
Success! You're on the list.

Baadhi ya viongozi wa mataifa makubwa duniani hasa Marekani wamekuwa wakikosoa jitihada mbalimbali zilizowekwa na shirika la afya duniani jinsi linavyokabiliana na janga hili la corona.

Mwezi Februari mwaka huu shirika la afya duniani lilisema kuwa katazo la kuzuia watu kusafiri halihitajiki katika kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu wa corona, tamko hili lilipuuzwa na mataifa mengi duniani

Mwezi Machi ilishutumiwa baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuzuia ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huu baada ya maafisa wakuu wa China kukataa kwenda Taiwan kujadili namna ya kudhibiti usambaaji wa ugonjwa huo.