HABARI

Yoweri Museveni: bado tunahitaji muda zaidi ‘siku 21 za marufuku ya kutotoka nje zaongezwa’

RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametangaza kuongeza muda wa siku 21 za kukaa katika kizuizi cha kutotoka nje kwa wananchi wa Uganda.

Hivi leo Rais Museveni katika mazungumzo yake na wanahabari kutoka ikulu ya rais na wanahabari kwa mkutano unaorushwa mubashara amesema kuwa bado wanahitaji muda ili waendelee kupambana na virusi hivyo na watu waendelee kusalia majumbani mwao.

“hawa 54 wamegundulika kwasababu tuliweka hatua za kuwazuia na kuwapima wasafiri wanaoingia nchini, kuna uwezekano baadhi ya wasafiri hawakuonesha dalili sasa hawa wataendelea kuambukiza watu wengine kwa siku 34 zijazo alisema Rais Museveni

Hatua hiyo imechukuliwa kama njia ya kuzuia ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini humo, mpaka sasa maambukizi ya ugonjwa wa corona yamefikia 54 huku watu wanne kati yao wakipona na hakuna kifo kilichoripotiwa kutokana na ugonjwa wa corona nchini humo.

Hapo awali serikali ya Uganda iliweka katazo la kutotoka nje kwa muda wa siku 14, kuanzia Machi 31 mpaka leo Aprili 14.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.